FAHAMU NAMNA NZURI YA KUVUNA MAJI YA MVUA KWA AJILI YA KILIMO NA MIFUGO

Katika maeneo mengi ya Afrika mashariki hususani Tanzania tuna kiasi kikubwa sana cha maji kwenye mito, chemichemi, maziwa na maji ya ardhini(undergroundwater) ambapo asilimia 70% hutumika kwenye kilimo kwa kuzalisha mazao mbalimbali Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi mvua iliyokuwa ikitegemewa sana na wakulima kama chanzo cha maji kwa mimea imekuwa sio ya kuaminika tena kwani hainyeshi tena kwa wakati, hunyesha kwa kiasi kidogo sana(450mm-600mm), maeneo mengine hunyesha kwa kiasi kikubwa sana mpaka kusababisha mafuriko ambayo huharibu vibaya mazao ya wakulima mashambani, pia baadhi ya vyanzo vya maji vimekauka na hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa maji sio tuu kwenye kilimo bali hata kwenye upatinaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani KWA NINI TUVUNE MAJI YA MVUA Kama nilipoeleza hapo awali kuwa kuna baadhi ya maeneo mvua hunyesha kwa kiasi kidogo sana na hivyo hazitoshelezi kumalizia msimu mzima ili...